Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemvua hadhi ya ubalozi Dkt Willibrod Slaa kuanzia jana Ijumaa Septemba 1, 2023.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu siku ya jana Bi. Zuhura Yunus.
Dk Slaa aliteuliwa kuwa balozi Novemba 23, 2017 katika uongozi wa awamu ya tano na kwa mujibu wa taarifa hiyo hakuna sababu iliyoelezwa kuvuliwa kwake wadhifa huo.
#KonceptTVUpdates