Droo ya makundi ya Ligi ya mabingwa Ulaya 2023/24 imekamilika rasmi usiku wa kuamkia leo tarehe 1 Septemba 2023 kwenye jiji la Monaco nchini ufaransa ambapo pot nne kila moja ikiwa na timu nane zilipangwa na hatimaye kupatikana makundi yote manne.
Mashindano hayo ambayo ni pendwa na yenye mafuatiliaji wengi Zaidi duniani yanatarajiwa kuanza rasmi tarehe 19/09/2023 na kutamatika kwa faianali ambayo itapigwa tarehe 01/06/2024.
Fainali hiyo ya msimu wa mwaka 2023/24 inatarajiwa kupigwa katika dimba la Wembley, nchini Uingereza ambapo kwa msimu uliomalizika fainali hizo zilifanyikia nchini Uturuki.
#KonceptTVUpdates