Nchi pekee barani Afrika iliyobakia na utawala kamili wa kifalme, Eswatini, Ijumaa wiki hii itafanya uchaguzi wa bunge huku vyama vya kisiasa vikiwa vimezuiwa kushiriki uchaguzi huo.
Katiba ya nchi hiyo inasisitiza juu ya kile kinachoitwa ”kigezo cha mtu binafsi” kama msingi wa kuchaguwa wabunge, ambao hawafungamanishwi na kundi lolote la kisiasa.
Kadhalika watu wanaokubalika kwa Mfalme Mswati wa Tatu mwenye mamlaka yote ya uongozi nao wako katika nafasi nzuri.
Takribani wapiga kura 585,000 waliojiandikisha watashiriki kuchagua wabunge 59. Bunge la Eswatini lina jukumu moja tu, ambalo ni kutowa ushauri kwa ufalme.
Nafasi ya vyama vya kisiasa haijafafanuliwa wazi nchini humo na ndio sababu haviruhusiwi kushiriki moja kwa moja katika uchaguzi.
#KonceptTVUpdates