Uongozi wa Fountain Gate Princess jana septemba 18,2023 umetoa ufafanuzi kuhusiana na tukio linalohusiana na aliyekuwa mchezaji wao, Penis Oside raia wa Kenya. Kupitia barua iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii ya klabu hiyo inasema.
Penis Oside alisajiriwa na Fountain Gate Princess mwezi Juni mwaka 2022 kwa kandarasi ya miaka miwili hadi May 2023 mkataba wake ukisitishwa kwa makubaliano ya pande zote mbili na aliagwa kwa taratibu zote na kupatiwa haki zake kama mkataba wake unavyotaka.
Tumepokea taarifa kuwa mchezaji huyo alikuwa na mahusiano na mmoja wa viongozi wetu na kwamba amempa ujauzito. Sisi kama taasisi tumechukua hatua ya kumuandikia barua mtuhurniwa na kumtaka kuandika barua ya kujibu tuhuma hizo. Mtuhumiwa ameandika barua na kupinga tuhuma hizo.
Taasisi imemsimamisha kazi mara moja mtuhumiwa kupisha uchunguzi. Pia imeendelea kuwasiliana na viongozi wa ‘Football Kenya Federation” (FKF), “ShIrikIsho la Mpira wa Miguu Tanzania’ (TFF) na familia kujua hatua zinazopaswa kufuatwa kuhusiana na jambo hii. Taasisi itaendelea kutoa ushinkiano wa dhati hadi ukwell ufahamike na hatua stahiki kuchukuliwa kwa muhusika.
Tunapenda ieleweke kuwa Fountain Gate Princess inapinga vikali tabia hii na imekuwa ikishirikiana na asasi za kiraia mbalimbali kwenye kutoa semina za mara kwa mara kwa wachezaji na viongozi na kuwapa nafasi wachezajl kuongea na uongozi wa juu kabisa kama kunaonekana kuwepo dalili zozote za unyanyasaji wa kijinsia au rushwa ya aina yoyote ile.
Pia wachezaji wetu wana ulinzi madhubuti na kusimamiwa na viongozi wa kike (matrons) wakati wote wawapo ndani ya kambi au nje ya kambi.
Hata hivyo ni vigumu kugundua table binafsi ya baadhi ya viongozi na nia ovu waliyonano. Hivyo Kwa hili lililotokea likithibitika ni tibia binafsi ya kiongozi na wala si msimamo wa Taasisi.
Taasisi itaendelea kutoa ushirikiano mpaka mwisho hivyo wote wanafuatilia jambo hili hadi ukweli utakapojulikana na adhabu stahiki kuchukuliwa ili liwe fundisho kwa viongozi wengine wenye tabia zinazofanana na hizi.
#KonceptTVUpdates