Mapema jana, wilayani Nachingwea, wananchi wa meshuhudia ujio wa gari maalum lenye vifaa vya kuvutia macho na masikio, kikiwa na jukumu la kusaidia kulinda mazingira na kuwalinda wakazi wetu wa porini. Gari hili lenye spidi, spika zenye kelele, na taa kali sana linatarajiwa kufanya kazi muhimu ya kuwaswaga tembo kutoka maeneo ya makazi yao kuelekea mbugani.
Akizungumza wakati wa utambulisho wa gari hilo kwenye Kijiji cha Mkoka, Wilayani Nachingwea, Mhifadhi Mkuu wa Kanda, Afande Linus Chuwa, alielezea umuhimu wa gari hili katika kusaidia askari wa wanyamapori. Alisema kuwa gari hili litatumia teknolojia ya ndege nyuki kutoa picha za maeneo ambayo tembo wapo na njia wanazotumia.
Gari hili litasaidia kudumisha amani kati ya binadamu na wanyama wa porini, na kwa kufanya hivyo, tutaweza kuendeleza uhifadhi wa mazingira yetu kwa vizazi vijavyo.
#tukovizuri
#KonceptTvUpdates