Hii leo septemba 21,2023 Haier ambao ni wazalishaji wa vifaa vya kielektroniki wameungana na Azam TV ambao hutoa burudani za runinga za kidigitali wamezindua rasmi kampeni mpya inayohusisha TV (runinga) za Haier Pamoja na visimbuzi vya Azam TV ili kuboresha utoaji burudani majumbani.
Ushirikiano huu unaashiria hatua muhimu kwa kampuni zote mbili katika kurahisisha utoaji burudani Tanzania. ambapo Teknolojia ya hali ya juu ya Haier katika vifaa vya nyumbani pamoja na utaalamu wa Azam TV katika utoaji wa burudani za kidigitali wameungana kuongeza tija kwa wateja na wasambazaji wa bidhaa hizi zote mbili.
Muungano huo utapatikana Kwa kuanzaia Shilingi 359,000 tu, ambapo mteja atajipatia TV kutoka Haier na kisimbuzi kutoka Azam chenye kifurushi cha mwezi mzima. Huduma hii itapatikana Tanzania nzima kuanzia mikoa ya Dar es Salaam, kanda ya kati, kanda ya ziwa, kanda ya kaskazini na kusini.
“Tuna furaha kubwa sana kuanza safari yetu katika kutoa suluhisho la kipekee katika ulimwengu wa burudani za runinga, Ushirikiano huu baina ya Haier na Azam TV ni uthibitisho tosha kwamba kampuni zote mbili ziko tayari kuboresha mahitaji ya wateja wao. Kwa kuunganisha nguvu zetu, tunalenga kufafanua upya jinsi familia zinavyopata burudani ndani ya nyumba zao,” amesema Ibrahim Kiongozi wa Haier.
Kwa upande wa Azam TV wamesema kuwa “Azam TV ina shauku na ushirikiano huu na jinsi ambavyo itawarahisishia watumiaji. Kampeni hii inaashiria dhamira ya Azam TV katika utoaji burudani ya kipekee na ubunifu wa TV za Haier kwenye vifaa vya nyumbani Tunaamini ushirikiano huu utatoa hamasa ya uboreshaji wa kutoa Burudani ya nyumbani na kuweka viwango vipya vya tasnia” alisema Adam Nondo wa Azam TV.
#KonceptTVUpdates