Wizara ya mambo ya ndani inasema zaidi ya 1,400 wamejeruhiwa vibaya, na majeruhi wengi zaidi wako katika majimbo ya kusini mwa Marrakesh.
Mfalme Mohammed VI alitangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa na kuamuru kupelekwa makazi, chakula na msaada mwingine kwa walionusurika.
Tetemeko hilo la kipimo cha 6.8 lilipiga Marrakesh na miji mingi Ijumaa usiku. Katika maeneo ya mbali ya milima, vijiji vizima vinaripotiwa kusambaratika.
Kutoka kaatika Milima ya Juu ya Atlas, 71km (maili 44) kusini-magharibi mwa Marrakesh – jiji lenye hadhi ya urithi wa dunia ambayo ni maarufu kwa watalii.
Lakini mitetemeko hiyo pia ilisikika katika mji mkuu wa Rabat, ulio umbali wa kilomita 350, pamoja na Casablanca, Agadir na Essaouira.
Idadi ya vifo inazidi kuongezeka na hadi sasa imefikia karibu watu 2,900 huku wengine zaidi ya 2,500 wakiwa wamejeruhiwa. Vikosi vya uokoaji vimeendelea bila kuchoka kuwatafuta manusura, lakini katika kijiji cha Tafeghaghte, ni hali ya huzuni ndio iliyotawala jioni ya siku ya Jumatatu ambapo miili ya nusu ya wakazi wapatao 160 ilipatikana.
Juhudi za vikosi vya uokoaji zimeshuhudiwa katika maeneo mbalimbali yaliyokumbwa na janga hilo ambapo askari wa Morocco kwa ushirikiano na mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka Mataifa ya Uhispania, Qatar, Uingereza na Falme za Kiarabu yamekuwa yakifanya kazi usiku kucha na kutoa huduma muhimu na za haraka kwa manusura.
Morocco imekuwa ikikosolewa kuchelewesha kutoa idhini kwa mashirika mengine ya uokoaji kuingia nchini humo ili kutoa msaada wao, na maafisa wa Ufalme huo wanasema uamuzi huo unalenga kuepuka mkanganyiko katika uratibu ambao wanadai “hautokuwa na manufaa yoyote”.
Mbinu hiyo ni tofauti na ile iliyochukuliwa na serikali ya Uturuki, ambayo ilitoa ombi la usaidizi wa kimataifa katika saa chache tu zilizofuata tetemeko kubwa la ardhi mapema mwaka huu, ambalo pia liliipiga nchi jirani ya Syria.
Mwanzilishi wa Kikosi cha waokoaji wasio na mipaka Arnaud Fraisse ameliambia shirika la habari la AP kuwa msaada zaidi ungeweza kuwasili haraka zaidi nchini Morocco ikiwa serikali ingetoa ruhusa. Na kuongeza kuwa takriban timu zipatazo 100 zenye jumla ya waokoaji 3,000 tayari wamesajiliwa na Umoja wa Mataifa.
#KonceptTVUpdates