Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Camillus wambura amesema hali ya usalama na ulinzi nchini ni shwari na salama kwa kipindi chote hapa nchini kwani kuna amani na utulivu unaoendelea.
IGP Wambura ameyasema hayo leo tarehe 04 septemba 2023 mbele ya Rais samia suluhu hassan kwenye ufunguzi wa kikao kazi cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania Oysterbay Polisi jijini Dar es salaam huku akiishukuru serikali kwa ushirikiano ambayo inauonesha kwa jeshi hilo.
Aidha Jeshi la Polisi limeanza maandalizi kwa ajili kusimamia Uchaguzi kwa kuwajengea uwezo Maafisa wake na Katika Mkutano huu litajadili na kuweka mikakati kwa ajili ya Chaguzi zijazo” amesema Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Camillus Wambura
IGP Wambura ameongeza kuwa “Katika kutekeleza Maelekezo yako uliyoyatoa katika Mkutano wa mwaka Jana Jumla ya Mifumo ya TEHAMA 16 imetengenezwa na imeanza kufanya kazi.”
#KonceptTVUpdates