Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amekutana na ujumbe kutoka Korea Kusini uliojumuisha viongozi wa makampuni makubwa ya madini yanayohusika na mnyororo wa thamani wa uzalishaji betri za magari ya Posco Holdings, Posco International, SK, Korea Zinc na LX International kupitia madini ya kimkakati (critical minerals).
Waziri Mkuu Majaliwa amewaeleza wawekezaji hao juu ya utayari wa serikali katika kushirikiana nao katika uwekezaji wao kwa kuweka mazingira mazuri ya kisera na kuboresha miundombinu ya usafirishaji kwa njia ya barabara, maji, reli na anga.
Kwa upande wake Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema ushirikiano wa Korea Kusini na Tanzania katika eneo hili la madini ya kimkakati litasaidia kuchochea ukuaji wa sekta ya madini na kuongeza mchango wa sekta ya madini katika Pato la Taifa na kuongeza pia wamezungumza mazungumzo ya awali na wawekezaji hao juu ya kubadilishana uzoefu wa kitaalamu pamoja na umuhimu wa kuongeza thamani ya madini hayo hapa Nchini ili kuongeza tija na kuchochea uchumi wa ndani sambamba na upatikanaji wa ajira za kutosha kwa watanzania.
Kwa upande wake Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema ushirikiano wa Korea Kusini na Tanzania katika eneo hili la madini ya kimkakati litasaidia kuchochea ukuaji wa sekta ya madini na kuongeza mchango wa Sekta ya Madini katika pato la Taifa .
Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini Balozi Togolani Mavula amesema ni fursa ya kipekee ya nchi ya Tanzania kulitumia vizuri soko la Korea Kusini kwa madini ya kimkakati na kwamba ubalozi wa Tanzania utaendelea kuratibu upatikanaji wa Wawekezaji wengi zaidi katika maeneo mbalimbali ya Sekta ya Madini.
#KonceptTVUpdates