Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara), Abdulrahman Kinana, amesema Tamasha la Kizimkazi limefanikiwa kuwa chachu ya kuimarisha Muungano.
Kinana ameyasema hayo jana Agosti 31, 2023, alipozungumza kwenye kilele cha Tamasha la Nane la Kizimkazi, Zanzibar.
Amesema, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kipindi cha miaka miwili na nusu ya uongozi wa nchi, amedhirisha uongozi ni kuonyesha njia katika nyanja zote.
“Nchi yetu imepata maendeleo makubwa katika nyanja zote,” amesema Kinana katika tamasha hilo lililopambwa na kazi za utamaduni, sanaa na kuhudhuriwa na halaiki ya watu.
Amesema, kwa ukubwa na umaarufu wa tamasha hilo, siyo shughuli ya Zanzibar tu, bali ni tukio ambalo limeweka misingi mizuri ya kuimarisha Muungano.
Amefafanua kwamba, tamasha hilo kwa mwaka huu limewavuta Watanzania wengi kutoka nje ya Zanzibar kushiriki, na siku zijazo wengi zaidi watamiminika Kizimkazi siyo tu kujionea bali kushiriki.
#KonceptTVUpdates