Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameshuhudia utiaji saini wa mkataba kati ya Ofisi ya Rais TAMISEMI na Kampuni ya Tumbaku ya Japan (JT Group) utakayoiwezesha kampuni hiyo kuendelea kutoa huduma za kijamii katika maeneo inayonunua zao hilo nchini.
Waziri Majaliwa ameshuhudia utiaji saini wa makubaliano hayo Jumatatu, Septemba 11, 2023 kwenye Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es Salaam.
Mkataba huo wa miaka mitatu wenye thamani ya shilingi bilioni 3.2 utaiwezesha kampuni hiyo kutoa huduma hizo kwenye sekta za afya, elimu, maji na uwezeshaji wananchi kiuchumi kwenye maeneo hayo.
#KonceptTVUpdates