Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mhe. Mama Mariam Mwinyi ameitaka jamii kujikita zaidi kwenye kilimo cha zao la Mwani kwani kina fursa nyingi za uchumi na maendeleo.
Mama Mariam Mwinyi ameyasema hayo jana septemba 6,2023 wakati akizungumza kwenye Mkutano wa Kimataifa unaojadili mifumo ya chakula barani Afrika katika mada ya nafasi ya Mwanamke kwa sekta ya kilimo na chakula, iliyofanyika ukumbi wa Selous jengo la ukumbi wa kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere.
Vilevile, amesema Taasisi ya ZMBF imewawezesha kiuchumi Wanawake wakulima wa Mwani baada ya kuwaweka pamoja vikundi 16 vya kina mama kila kikundi watu 20 kwa Unguja na Pemba kwa kuwapa mikopo nafuu ili kuendeleza zao hilo.
#KonceptTVUpdates