Mchezo wa mzunguko wa pili wa klabu bingwa Afrika ambao utaikutanisha klabu ya Yanga SC kutokea nchini Tanzania dhidi ya Al Merrikh SC kutokea sudan rasmi utapigwa katika dimba la Kigali Pele Stadium pale nchini Rwanda.
Mchezo huo utapigwa tarehe 16 ya mwezi septemba mwaka wa 2023 ambapo mshindi wa mchezo huo na utakaofuata wa marudiano atasubiri kupangwa hatua ya makundi ya mashindano hayo ya klabu bingwa barani Afrika.
Taarifa za mchezo huo zimetolewa kwenye kurasa za mtandao ya kijamii wa klabu ya Yanga kutoka nchini Tanzania siku ya leo tarehe 02 septemba 2023.
#KonceptTVUpdates