Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania Hassan Mwakinyo ameendelea kushikilia msimamo wake dhidi ya pambano ambalo lilipangwa lifanyike leo ijumaa septemba 29,2023 dhidi ya mpinzani wake kutoka nje ya nchi ambapo awali ilkuwa ni bondia kutoka nchini kenya na baadae kudaiwa kubadilishwa kw ana kuletwa bondia kutoka nchini Namibia.
“Binafsi!! Napenda sana Kushukuru M/mungu kwa uzima na Afya nilio nayo Leo pia niwashukuru sana washabiki zangu kwa kujitokeza kwa Nguvu kuonyesha shauku ya kuni support nawashukuru sana AZAM TV kwa kuendelea kutoa nafasi!!
Kwetu kama wachezaji wa ndani naomba niweke hisia zangu wazi kwa mashabiki ya kuwa kesho sitaweza kupanda ulingoni kutokana na uwongo na udanganyifu, wa ma promota binafsi sina tatizo na Mtu ila pia naheshimu sana kazi yangu na siko tayari kuona watu wana nijaribu au kutaka kuharibu jina langu.
Azam nia na dhamira yenu ni njema sana kwenye mchezo wa ngumi na kwa nidhamu ya juu kabisa maamuzi ya hili kuendelea yako mikononi kwenu hapa tulipofkia nyinyi binafsi ndio mnaweza kutatua hii changamoto na Muda ni Leo tu.” Amesema bondia Mwakinyo.
Aidha Mwakinyo amesema mpaka hivi sasa nafasi ya yeye kushiriki pambano hii leo bado nid ndogo sana.
“Maswali na simu zimekua nyingi, kiukweli mpaka sasa nina asilimia 5% tu za kupanda ulingoni ikiwa zitaongezeka ni mimi mwenyewe nitasema naomba tuwe wavumlivu epuka matapeli…msimamo ni mmoja tu kama mogadishu… kwa kitendo hichi naomba!! huu ndio uwe mwisho wa mapromoter dhulma wahuni wadanganyifu na matapeli” ameongeza hii leo.
#KonceptTVUpdates