Mahakama ya Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma imemhukumu mshitakiwa Fabiani Yeronimo(40) kwenda jela miaka 30, ambaye ni mkulima na mkazi wa Kijiji cha Nengo wilayani Kibondo baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka Bibi (68) ambaye jina lake limehifadhiwa ambapo ni mkulima na mkazi wa Nengo.
Mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo Mei 16,2023 huko katika Kijiji cha Nengo wilayani Kibondo Mkoa wa Kigoma na kufikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Mei 22,2023.
Akitoa hukumu hiyo jana Septemba 5, 2023 hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Kibondo Mhe. Maila Makonya amesema kuwa mahakama imejiriridhisha pasipo na shaka ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na hatimae kumtia hatia mtuhumiwa huyo.
#KonceptTVUpdates