Muda ulikuwa umeenda sana macho ya KIM yalianza kufumba yenyewe ishara kuwa mwili wake ulikuwa umechoka na ulihitaji kupumzika. Saa yake ya ukutani ilionesha kuwa ilikuwa ni saa 8 usiku na alikuwa anasoma story pendwa inayoitwa BUSU LA SHAVUNI.
Nia ya kusoma story hiyo usiku ni kupunguza mlundikano wa mawazo aliyokuwa nayo na kutafuta faraja kupitia matatizo ya wengine.
Ni siku ya 6 tangu asimamishwe kazi kutokana na tuhuma za uwongo ambazo boss wake alijaribu kumbambikizia. Si kusimamishwa kazi tu bali pia mke wake kuondoka nyumbani kwa madai kuwa amemchoka. Ilikuwa haimuingii akilini kuwa eti mke wake amechoka na kuamua kumuacha katika kipindi hiki kigumu?
“Kwanini hakunichoka kipindi nikiwa nina kazi? kwa nini hakuondoka kipindi hicho? nini kimemfanya aondoke?” KIM aliwaza bila kupata majibu. Usingizi kwake ulikuwa ni mgumu sana na alitamani hata asilale.
Mziki wa taratibu ulitosha kabisa kuelezea ni jinsi gani alivyokuwa anajisikia. Machozi yalitosha kabisa kulowanisha karatasi za kitabu cha story alichokuwa anasoma.
Badala ya kufuatilia kitabu hicho ambacho kilikuwa ni kizuri alikuwa amekishika kama pambo na wala alikuwa haelewi kilichoandikwa. Alikuwa na huzuni iliyopitiliza. Alitamani hata kama asubuhi ingefika alione jua, akihisi labda kuliona jua kungefanya roho yake kutulia.
Mvinyo wa kizungu aliokuwa anakunywa hakuweza hata kuusikia, alikunywa kama maji.
Alikunywa lakini hakulewa. Kila alipokuwa anavuta kumbukumbu ya yaliyomtokea alilia kilio kisicho na machozi. “Nilimpa kila kitu nilimpenda kupita vitu vyote lakini leo ananiacha?” aliwaza bila kupata majibu.
Mwanamke huyo alikuwa ni kila kitu kwake kwani alimtoa mbali, mwanamke huyo alikuwa na umuhimu sana maana kwake alikuwa kama mama na hii ni baada ya kumpoteza mama yake mzazi ambaye alifariki dunia.
“Huyu mwanamke nilimsomesha kwa gharama zangu huyu mwanamke nilimwinua kutoka familia masikini mpaka akafikia hapo alipo. Hiyo kazi anayoringia ni sawa tu mimi ndio niliyomuwezesha kwa maana bila elimu niliyomsadia kuipata asingekuwa hapo. Lakini kwa nini sasa hataki kuyatambua hayo. Kwa nini hathamini mchango wangu kwake?”.
KIM aliongea kwa nguvu utafikiri labda huyo mwanamke wake alikuwa hapo. Alinyanyua glass ya kinywaji kikali alichokuwa akinywa na kunywa utadhani sio kilevi. Mara simu yake iliita na aliangalia kwa haraka maana sio kawaida yake kupigiwa simu usiku. Aliichukua simu ambayo ilikuwa kwenye chaji na kuipokea.
SIM… “Hello mambo KIM” ilisiskika sauti nyororro sauti ya kike iliyojaa bashasha na furaha.
KIM… “Poa, sijui naongea na nani?”.
SIM… “Jamani mbona unaharaka hivyo, mimi najua hunijui lakini utanijua maana ni zaidi ya malaika niliyetumwa na Mungu nije kukukomboa na kukuondoa kwenye upweke uliokuwa nao”.
KIM alijibu kwa hasira na kukata simu… “Makubwa kumbe kuna binadamu malaika. Utanisamehe kama huwezi kujitambulisha sitoweza kuongea na wewe.”
Kama hiyo haitoshi aliamua kuizima kabisa, alivurugwa akavurugika. Alihisi kabisa walikuwa ni vibaraka wa mkewe PAMELA walitumwa kumkejeli. Pamoja na kuwa alichukua maamuzi hayo bado roho ilimsuta kwa jinsi sauti hiyo ya kike ilivyokuwa tamu masikioni mwake. Alitamani sana kumjua mwanamke huyo lakini hakutaka kuwasha simu.
Alijitupa kitandani na kuanza kuutafuta usingizi ambao takribani wiki nzima alikuwa akiupata kwa shida sana. Aliendelea kuwaza vitu vingi sana ikiwa ni Pamoja na atapata wapi pesa ya kodi kwa sababu mwezi huo ndo ulikuwa wa kulipa kodi ilihali amesimamishwa kazi kwa sababu ambazo ni za kusingiziwa.
“Yaani Boss Yule mwanamke ni mchepuko wake tu je ingekuwa ni mke wake si angenifunga jela kabisa. Mwanamke mwenyewe hamtaki anataka vijana wenziye yeye kazi kuonga tu. JENI ametamka kwa kinywa chake kuwa hampendi boss bali mimi sasa mimi ningefanyaje.
Yaani mwanamke mzuri kama JENI amejilengesha mwenyewe mimi nimwache kisa eti ni mchepuko wa boss ambaye hajawahi kulala naye?”. KIM aliendelea kuwaza na kuwazua.
“Pengine mke wangu alijua yote haya yanayoendelea kazini? Na kwa nini hakuniuliza akaamua kuondoka kimya kimya bila hata kuniambia sababu. Nimepiga simu mpaka nyumbani kwao hawapokei tatizo ni nini hasa?”.
Maswali yote hayo hayakuwa na majibu kwa kijana huyu. Alifikiria jinsi ya kupata kazi ilivyokuwa ngumu. Alifikiria kuwa hata kazi hiyo aliipata kwa msaada wa mjomba wake. Ni kweli elimu yake ilikuwa nzuri kuliko wafanyakazi wengine na hata utendaji wake wa kazi ulikuwa na ufanisi mkumbwa kuliko wengine.
Tatizo kubwa ni mfanyakazi mpya wa mambo ya masoko aliyeletwa hapo kazini kwao. Msichana huyu alikuwa mrembo kupita kiasi. Urembo wa JENI ndo huo ulileta kizaazaa katika taasisi yao. KIM ni mfanyakazi wa benki moja ya kibiashara mkoani DODOMA.
Ni miezi 3 tu tangia apate kazi hiyo na katika muda huu mfupi ndo analetwa JENI binti ambaye alimvutia kila mwanaume hapo benki.
Boss naye alikuwa mtu aliyevutiwa na mfanyakzi huyo na yeye alitumia cheo chake kumshawishi na kutaka kuwa naye. Lakini JENI alikuwa ni mwanamke mjanja sana bado aliangalia future yake. Ni msichana ambaye hakupenda kujihusisha kimauhusino na wazee.
Lakini moyo wake ulivutiwa na kijana KIM ambaye alikuwa ni kipenzi cha wafanyakazi wengi na wateja kutokana na ufanisi wake wa kazi kuwa uliotukuka. Hali hii ilijenga ukaribu sana na kupeleka kujikuta wakizama kwenye uhusiano bila kutajaria.
JENI alijua kabisa kuwa KIM alikuwa na mke ambaye naye ni mfanyakazi wa taasisi nyingine hapo hapo DODOMA. Wote waliingiwa na upofu ambao kwa kweli ulileta majanga makumbwa kwa upande wa KIM.
KIM alijiuliza kama walifanya siri yeye na JENI imekuwaje mke akajua na kuamua kuondoka. Mkewe aliondoka ghafla bila kutoa sababu yoyote na kipindi hiko tayari alishasimamishwa kazi kwa kile kilichoitwa ubadhilifu wa fedha.
Kitu kingine kilichokuwa kikimuuma ni kuwa Boss na mkewe walikuwa wakijuana maana walitoka mkoa mmoja na walikuwa karibu.
KIM alihisi labda Boss ameamua kumwaga sumu kwa mkewe na ndio maana ameondoka. Alichokifanya alilala na asubuhi na mapema aliamka na kuelekea ukweni ambapo ni BAGAMOYO.
Aliamua kwenda ili kujua kama mke wake alirudi huko au laa kuna sehemu ambayo alienda bila yeye kujua. Ila ile simu alivyoiwasha asubuhi hiyo alikutana na meseji nyingi za yule mwanamke aliyempigia simu usiku huku akijichekesha chekesha.
“KIM najua upo katika kipindi kigumu sana, kipindi cha mawazo lakini mimi ndo naweza kukufumbua macho na kujibu maswali yako yote magumu yanayokutatanisha. Hata mimi nina maumivu sana ila naomba tushirikiane nitakufuta machozi na pia nitakufanya ujue ukweli kuhusu mkeo na boss wako. Ukiwa tayari tafadhali nitafute naitwa MAMA T.”
Meseji ilisomeka hivyo na kumfanya KIM azidi kuchanganyikiwa. Alitamani kushuka kwenye gari lakini aliamua kuendelea na safari ya ukweni maana ingetoa mwanga pia kwa nini mkewe aliamua kuondoka tena kimya kimya…
Huyo alifika MOROGORO na kupanda gari la kuelekea BAGAMOYO. Alifika ukweni na alipokelewa na baba mkwe. Alipokelewa vizuri tofauti na alivyotarajia hapo awali. Na baadaye alikuja mama mkwe.
MAMA… “Karibu sana mwanangu naona umefanya ziara ya kushtukiza”
KIM… “Ni kweli mama angu sijui mnaendeleaje maana nimekuwa nikipiga simu kwa muda mrefu mmekuwa hampokei”.
BABA alidakia… “Tusamehe tu baba si unajua huku shughuli za shamba zinatubana hatuna hata habari na hizo simu”
Kimya kilitawala kidogo kabla ya KIM kutaka kuzungumza ili kuvunja ukimya huo.
KIM… “Wazee wangu mimi nimekuja kuwasalimu lakini pia mwenzangu aliondoka wiki sasa imepita bila kuaga sijui alifika huku kwenu?”
MAMA alijibu kwa hisia… “Hapana mwanangu PAMELA hajafika huku ila mara ya mwisho kuongea naye alisema kuwa umebadilika. Umekuwa Malaya na unahangaika na mapenzi nje ya ndoa. Pia kuna mwanamke kazini kwako anakuchanganya na umeapa kumuoa.
Mwanetu amesema kuwa hayupo tayari wewe umletee magonjwa hivyo amejitoa kwako. Ameamua kuanza maisha yake na sisi utaratibu wetu ni kuwa mwanamke akishaolewa basi akae huko kwa mme wake na wakaichana asirudi nyumbani atafute mwanaume mwingine wa kumuoa.”
INAENDELEA……………….EP 02
SOURCE: http://deusdeditmahunda.blogspot.com
#KisamkasaKonceptTVUpdates