Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo septemba 26, 2023 amemuagiza mkurugenzi mtendaji mpya wa shirika la umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga kushughulikia tatizo la umeme kwa muda wa miezi sita.
Ameyasema hayo Ikulu ya Dar es salaam alipokuwa akiwaapisha viongozi mbalimbali aliowateuwa na wengine kuwabadilishia majukumu siku za hivi karibuni.
Aidha Rais Samia amesema kukatika kwa umeme sio tatizo la mtu mmoja badala yake ni tatizo la kitaifa kutokana na usafishwaji wa mitambo Pamoja na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yamepelekea maji kupungua kwenye vyanzo vya uzalishaji umeme.
#KonceptTVUpdates