Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa-2023 zimetembelea na kukagua uhifadhi wa chanzo cha maji cha Ivumwe Wilaya ya Mbeya mjini. Chanzo hicho kina uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 29 kwa siku.
Kiongozi wa Mbio hizo ameipongeza Bodi ya Maji ya Bonde la Ziwa Rukwa kwa kuendelea kutunza na kuhifadhi chanzo hicho kwa upandaji wa miti rafiki wa maji ipatayo 490.
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) katika mbio hizo amesisitiza kuwa wakazi wa Kata ya Mwakibete waendelea kutunza na kulinda chanzo cha maji pamoja na mazingira yake kwa ujumla ili kuhakikisha huduma ya maji inakuwa endelevu.
Amesema kuwa katika kuboresha huduma ya maji katika jiji la Mbeya, Serikali kwa mwaka 2023/24 inaendelea na utekelezaji wa mradi wa maji wa Mto Kiwira kwa gharama ya shilingi bilioni 117 ambapo mpaka sasa shilingi bilioni 14.9 zimetolewa ikiwa ni malipo ya awali kwa kazi hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Tulia Ackson ameishukru Serikali kwa utekelezaji wa miradi ya maji katka Jiji la Mbeya ukiwemo mradi wa maji wa Mto Kiwira.
Amesema kuwa chanzo cha maji cha Ivumwe ni muhimu na kinatumika kwa ajili ya usambazaji maji kwa wakazi wa mitaa ya Forest mpya, forest ya Zamani, Mwanjelwa, Old airport, Iyela, Iyunga, Iwambi, Viwanda vya Coca-Cola, Veta pamoja na mtaa wa Nane nane.
#konceptTVUpdates