Mapema hii Leo septemba 13,2023 shirikisho la soka Tanzania limeingia makubaliano rasmi na kituo cha runinga cha TV3 kuonyesha ligi ya NBC CHAMPIONSHIP LEAGUE ambapo Mkataba huu na TV3 utakuwa wa miaka mitatu na thamani ya mkataba huu ni milioni 613 Tsh ukisainiwa na Rais wa soka Tanzania TFF Wallace Karia.
Rais Karia amesema “watakuwa Pamoja na uongozi wangu sisi ni waungwana na thamini Tv3 kuja wakati Championship ikiwa katika kipindi kigumu…hivyo mtaendelea kuwa kipaumbele chetu kwa miaka ijayo…baadae mambo yakiwaka… Najua watu watakuja…lakini sisi tutawapa kipaumbele TV3.”
Ameendelea kwa kusema kuwa “Lgi ya NBC Championship itakayokuwa inarushwa Na Tv3 na TV3 Sports, nadhani dunia wataona Championship ni Ligi ngumu kuliko hata Ligi yetu kuu…Pia itatusaidia kuepusha mambo ya ajabu kwani kila kitu kitakuwa hadharani… Tv3 itafika mbali na Championship itafika mbali pia. Mkataba huu ni wa miaka 3 wenye thamani ya milioni 613 za kitanzania…” Wallace Karia Rais wa TFF.
Tv3 hamtojuta kuchukua Ligi hii…kwani hata viwanja ni vya viwango stahiki..Viwanja ambavyo havitokidhi vigezo havitotumika kwenye NBC CL kama ilivyo katika Ligi Kuu…Kwa hio hii itawapa fursa ninyi TV3 kurusha matangazo kwa picha HD kama mlivyokusudia” Wallace Karia Rais wa TFF.
#KonceptTVUpdates