Benki ya NMB imezindua dirisha la pili la Nuru Yangu scholarship and mentorship program ambayo lengo lake ni kufadhili masomo ya shahada ambapo hutolewa kwa wanafunzi wenye ufaulu mzuri kwenye mitihani ya kidato cha sita lakini wanatoka kwenye mazingira magumu na hawana uwezo wa kujisomesha kwa mwaka wa masomo 2023/24.
Uzinduzi huu umefanywa na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NMB Foundation – Bi. Ruth Zaipuna pamoja na Meneja Mkuu wa NMB Foundation – Nelson Karumuna ambapo Zaidi ya ufadhili wa masomo, vijana hawa watapata mafunzo ya vitendo katika benki ya NMB na makampuni mengine washirika.
Kwa mwaka huu, NMB imetenga zaidi ya Tsh Bilioni 1 kwaajili ya wanafunzi 130 (65 wa mwaka jana na 65 wa mwaka huu) kugharamia Ada, Fedha za Kujikimu, Fedha kwaajili ya mafunzo kwa vitendo, Gharama zote zinazolipwa kwa chuo, Vifaa vya shule na Kompyuta mpakato (laptops).
#KonceptTVUpdates