ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Tuesday, October 3, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

NMB yashinda tena tuzo ya kuongoza kuwafadhili wajasiriamali – Afrika

I am Krantz by I am Krantz
Sep 19, 2023
in HABARI
0
NMB yashinda tena tuzo ya kuongoza kuwafadhili wajasiriamali – Afrika
0
SHARES
19
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Benki ya NMB imetunukiwa tena tuzo na jukwaa la kufadhili ujasiriamali duniani (SME Finance Forum) kutokana na huduma zake wezeshi na ufadhili wake wa kuwaendeleza wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini wakati wa mkutano wa jukwaa hilo uliofanyika September 14 katika jiji la Mumbai nchini India.

Ushindi iliyoupata Benki hiyo kwenye tuzo za mwaka huu za ufadhili wa ujasiriamali duniani (Global Finance Awards 2023 – GSMEFF 2023), ni wa Mfadhili wa Ujasiriamali wa Mwaka upande wa Afrika uliyoipa tuzo ya fedha (Silver Award).

RelatedPosts

KANISA LAPOROMOKA MEXICO NA KUUWA WATU 10

KANISA LAPOROMOKA MEXICO NA KUUWA WATU 10

Oct 2, 2023

TAKRIBAN WAHAMIAJI 10 WAMEFARIKI NA WENGINE 25 KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA LORI NCHINI MEXICO

Oct 2, 2023

AIRPORT YA ZANZIBAR IPO BUSY KULIKO YA DAR ES SALAAM

Oct 2, 2023
Load More

Kama ilivyokuwa kwa tuzo zingine, tuzo za GSMEFF 2023 zinatambua dhamira na mafanikio ya taasisi za kifedha na kampuni zinazojihusisha na teknolojia za huduma za kifedha (fintech) katika kuwahudumia wateja wao ambao ni wajasiriamali wadogo na wa kati.

 

Pamoja na mambo mengine, tuzo hii imetambua mchango wa NMB katika kuwawezesha wajasiriamali kukuza biashara zao kwa: Kuwapa mikopo yenye riba nafuu kwa wakati, kuwapa elimu ya fedha kuhusu jinsi gani watazidi kukuza biashara zao kupitia majukwaa yao ya Business Clubs, Business Executive Network na mengine. Pia, kuwawezesha kupokea malipo kidijitali kupitia NMB Lipa Mkononi na njia zingine za kidijitali, kuwawezesha kukopa kidijitali bila kuwa na dhamana yoyote kupitia huduma ya Mshiko Fasta na kuendelea kufurahia huduma za kibenki kwa urahisi kupitia NMB Mkononi na Wakala popote pale wanapokuwa

 

Heshima hii ni ushahidi mwingine wa juhudi za dhati za benki hiyo za kuziba pengo la kuwafadhili wajasiriamali na uwekezaji inaoufanya katika uvumbuzi wa kidijitali nchini. NMB inazingatia maendeleo ya wafanyabiashara hao kutokana na mchango wao mkubwa katika ujenzi wa Taifa kwa kutengeneza ajira, kuchochea ukuaji wa uchumi na kuimarisha mapato ya wananchi.

Tuzo hizi na heshima iliyopata NMB ni ushahidi wa mwendelezo wa ubora wa huduma na dhamira ya dhati ya ubunifu wake.

 

Katika pongezi zake kwa washindi, Afisa Mtendaji Mkuu wa jukwaa la kufadhili ujasiriamali duniani (SME Finance Forum), Bw. Matthew Gamser, alisema ushindani wa mwaka huu ulikuwa mkubwa kutokana na washiriki kuwa wengi wakitoka katika nchi nyingi ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

 

SME Finance Forum, inayoratibiwa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) la Benki ya Dunia, ilianzishwa mwaka 2012 na nchi 20 tajiri duniani (G20) chini ya mwamvuli wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Ujumuishaji wa Kifedha (GPFI).

 

Majukumu yake makubwa ni pamoja na kusimamia wanachama wake kubadilishana maarifa, kuchochea ubunifu na kukuza ukuaji wa wajasiriamali.

 

Related

I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

KANISA LAPOROMOKA MEXICO NA KUUWA WATU 10
HABARI

KANISA LAPOROMOKA MEXICO NA KUUWA WATU 10

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023
HABARI

TAKRIBAN WAHAMIAJI 10 WAMEFARIKI NA WENGINE 25 KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA LORI NCHINI MEXICO

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023
AIRPORT YA ZANZIBAR IPO BUSY KULIKO YA DAR ES SALAAM
HABARI

AIRPORT YA ZANZIBAR IPO BUSY KULIKO YA DAR ES SALAAM

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023
MIFUMO YA KIFEDHA KULINDWA ZAIDI
BIASHARA

MIFUMO YA KIFEDHA KULINDWA ZAIDI

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023
SIKU 7 ZATOLEWA MILANGO KUBADILISHWA
HABARI

SIKU 7 ZATOLEWA MILANGO KUBADILISHWA

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023
TWENDE BUTIAMA YAANZA RASMI KUTOKA DAR MPAKA BUTIAMA
HABARI

TWENDE BUTIAMA YAANZA RASMI KUTOKA DAR MPAKA BUTIAMA

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

September 2023
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930  
« Aug   Oct »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In