Jeshi la polisi nchini limetoa taarifa kwa umma juu ya mabadiliko ya namba ya simu ya mokononi ya mkuu wa jeshi la polisi nchini (IGP) ambayo wananchi walikuwa wakitumia kumpigia pale wanapohitaji msaada au kufikisha malalamiko.
Namba hiyo iliyokuwa imewekwa katika vituo vyote vya Polisi awali ilikuwa ni 0684111111 ambapo haitotumika tena kuwasiliana na mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania.
Namba mpya ambayo itatumika kuanzia hivi sasa ni 0699998899 na itakuwa inapatikana wakati wote, usiku na mchana na imekwishwa kuwekwa kwenye vituo vyote vya Polisi nchini.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wote kutumia namba hiyo kwa ajili ya mambo muhimu ambayo wataona hakuna msaada mwingine kuanzia ngazi ya kituo Zaidi ya kumpigia yeye.
#KonceptTVUpdates