Marekani inasema kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un anatarajia kukutana na rais wa Urusi Vladimir Putin kuzunumzia juu ya kuipelekea silaha Urusi kwa ajili ya vita vyake nchini Ukraine.
Tangazo hilo limetolewa baada ya ikulu ya Marekani kutahadharisha wiki iliyopita kwamba Urusi kwa njia ya siri ilikuwa tayari ikifanya mazungumzo na Korea Kaskazini kupata silaha kadhaa na mahitaji mengine kwa juhudi zake za vita.
Kwa mujibu wa gazeti la Marekani la The New York Times Kim huenda akasafiri mwezi huu kwenda Vladivostok mji wa pwani ya bahari ya Pasifiki ambao hauko mbali sana na Urusi, kukutana na rais Putin.
Gazeti hilo aidha limeripoti kuwa Kim jJong Unhuenda hata akasafiri kwenda mjini Moscow, lakini hilo halina uhakika. Urusi na Korea Kaskazini hazijasema lolote kuthibitisha mkutano kati ya viongozi wao.
Tutumie maoni yako
Kuna wasi wasi huko Washington na Seoul juu ya kile ambacho Korea Kaskazini itapata kwa makubaliano kama hayo, ambayo yanaweza kusababisha kuongezeka kwa ushirikiano wa kijeshi kati ya nchi hizo mbili za Asia.
Siku ya Jumatatu, idara ya ujasusi ya Korea Kusini iliarifu kwamba Bw Shoigu alipendekeza Urusi, China na Korea Kaskazini zifanye mazoezi ya pamoja ya wanamaji, sawa na yale yaliyofanywa na Marekani, Korea Kusini na Japan.
Hofu nyingine ni kwamba Urusi inaweza kuipatia Korea Kaskazini silaha katika siku zijazo, wakati ambapo Pyongyang inazihitaji zaidi.
Kinachotia wasiwasi zaidi bado, Kim Jong Un anaweza kumwomba Bw Putin kumpa teknolojia ya hali ya juu ya silaha au maarifa, ili kumsaidia kufanikiwa katika mpango wake wa silaha za nyuklia.
#KonceptTVUpdates