Rais wa jamhuri ya Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka Majaji wafikishe huduma na kutenda haki kwa Wananchi huku wakitumia weledi na ujuzi wao wote kuwatendea vyema wananchi kupitia mahakama.
Rais Samia ameyasema hayo jana septemba 14, 2023 wakati wa uapisho wa majaji, makatibu wakuu, naibu katibu mkuu na naibu mwanasheria mkuu wa serikali uliofanyika ikulu jijini dar es salaam.
Aidha Rais Samia amesema kuwa kuteuliwa kwao ni kwa ajili ya Kwenda kuongeza utendaji kwa wananchi na kuongeza Imani ya mahakama kwa wananchi.
#KonceptTVUpdates