Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania samaia suluhu hassan hii leo septemba 1,2023 amewaapisha mawaziri na manaibu wake ambao taarifa za uteuzi wao zilitolewa tarehe 30 augosti 2023 kwenye ukumbi wa Ikulu ndogo Tunguu, Zanzibar.
Rais samia amewaasa wapya kwenye safu hiyo ya uteuzi Jerry, Kapinga, Kipenzile, Mnyeti, Kitandula…nyinyi ni wapya kabisa, nadhani mnayaona yanayotokea Bungeni na mmekuwa mkipaza sauti kubwa kwa Mawaziri kule Bungeni, sasa exactly yale mliyokuwa mkiyapazia sauti mnakwenda kuyafanya nyinyi, wanasema ukitaka uhondo wa ngoma ingia ucheze…sasa mko kwenye ngoma tunatarajia mcheze kwelikweli na mle mabadiliko mliyokuwa mnayahoji kule” Rais Samia Suluhu Hassan
Aidha rais samia amesema Waheshimiwa Mawaziri na Makatibu Wakuu na viongozi wote mliopo hapa sisi ni watumishi wa watu, sasa kuna mwingine akipata appoitment, anajiona sasa yeye, atanijua mimi ni nani…katika utumishi wa watu, mahusiano ni jambo zuri sana, sasa ukijipandisha…unataka kukaribia mbinguni kwamba umepata uteuzi…hutatumikia watu, naombeni sana upole si ujinga hata kidogo…saa nyingine ndio maarifa.
#KonceptTVUpdates