Serikali kupitia Wizara ya Afya imesema imeunda Programu Maalum ya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa yasiyoambukiza (Tanzania NCD Prevention and Control Program TaNCDP) ndani ya Idara ya Tiba ambayo ina jukumu la kuandaa miongozo na mikakati ya kisekta kwenye mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza.
Hayo yamebainishwa leo septemba 4,2023 Bungeni na Naibu Waziri, wa Afya Dkt. Godwin Molel wakati akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Manyoni Mashariki, Dkt. Pius Stephen Chaya aliyeuliza lini Serikali itaanzisha Mamlaka ya Kuratibu na Kupambana na Magonjwa yasiyoambukiza.
Dkt. Mollel amesema kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu imekwishatekeleza jukumu hilo kwa kukiongezea jukumu Kitengo cha Afya Moja (One Health) kusimamia Magonjwa yasiyoambukiza chini ya Kurugenzi ya Menejimenti ya Maafa.
Aidha akijibu swali la nyongeza Dkt. Mollel amesema kuwa serikali chini ya Rais Samia itatumia wahudumu wa afya ngazi ya jamii kutoa hamasa na elimu ya uelewa juu ya kujikinga na magonjwa yasiyoyakuambukiza ili kuhakikisha elimu sahihi inafika kwa wananchi wa ngazi ya msingi.
#KonceptTVUpdates