Kutembea kama bata: Aina hii ya utembeaji inasaidia kuimarisha miguu na kifanya kuwa myepesi, inaondoa maumivu ya uti wa mgongo. Inakuwa na ufanisi zaidi ukiwa unafanya kwa dakika 3 hadi 5 kwa siku.
Kujikunja kama mtoto ndani ya tumbo la mama: Namna hii ya kujikunja inasaidia kupunguza hali ya kuvimbiwa, inasafisha uchafu ndani ya utumbo mpana, inakuwezesha kulala vizuri. ufanisi wake ni pale utakapofanya kwa dakika 15 kwa siku.
Kuning’iniza mwili, aidha kwa kubembea ukiwa umeshikilia sehemu iliyo juu: Hii inasidia kunyoosha mgongo na kupunguza kisha kundoa maumivu ya uti wa mgongo, inanyooha na kumarisha mgongo, inasaida mabega na shingo kuwa katika hali ya msawazo. Ifanye kwa sekunde 20 mara 3 hadi 6 kwa siku.
Kuruka ruka kama unaruka kamba: Kunasidia kupunguza kitambi, huboresha afya ya tezi dume, hufungua mgongo ili kunyumbulika zaidi. Inapendeza zaidi ukiruka mikupuo 9 mara 3 kwa siku.
Mtu ni afya zingatia afya yako hata ufanisi wa akili yako utakuwa mkubwa zaidi kwakuwa una afya nzuri.
#KonceptTvUpdates