Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amesema kuwa soko la Mabibo linatarajiwa kuingiza bilion 2 kufikia mwisho wa mwaka baada ya kuweka usimamizi mzuri wa makusanyo, Hali hii imekuja mara baada ya awali fedha za ushuru na kodi katika soko hilo kuishia mifukoni mwa watu wasio waamini.
Ikumbukwe kuwa wiki chache zilizopita mkuu huyo wa mkoa albert chalamila alifuta uongozi wa soko la mabibo mara baada ya kufanya mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya soko la mabibo kufuatia utendaji mbovu wa waliokuwa viongozi wa soko hilo la mabibo.
“Napenda kukujulisha Mhe Rais soko letu la Mabibo tunatarajiwa mpaka mwisho wa mwaka litaingiza bilion 2 baada ya kuweka usimamizi mzuri na kuondoa wale waliokuwa wakichukua fedha na kutoziwasilisha” amesema Chalamila.
Ameyasema hayo hii leo tarehe 04 septemba 2023 kwenye ufunguzi wa kikao kazi cha maafisa wa jeshi la Polisi kinachotarajiwa kuanzia leo Polisi Oysterbay ambapo wataangazia hali ya utendaji na maboresho ya utendaji wa jeshi hilo
#KonceptTVUpdates