Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson amesema ni wakati sasa wakufanya tathmini Maalum ya mfumo unaotumika kuagiza mafuta kwa Pamoja wa ili kuona ni sababu zipi zinasosababisha changamoto ya upatikanaji wa mafuta.
Mhe. Dkt. Tulia ameyasema hayo leo septemba 7,2023 Bungeni jijini Dodoma ambapo amesema kuwa kabla ya mfumo huo wa Sasa hapo awali kulikuwa na mfumo ambao ulikuwa unatumiwa ambao sasa hautumiki.
Amesema kama mfumo huo unaleta changamoto basi warejee katika mfumo wa zamani kwa kuboresha maeneo yaliyokuwa na changamoto, lakini kama mfumo wa sasa nao unaonekana ni sahihi basi waangalie maeneo yenye changamoto parekebishwe.
#KonceptTVUpdates