Ofisi ya Rais -TAMISEMI imeona taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuhusisha mwanafunzi SIFIKA DANIEL RUBEN aliyesoma Shule ya Sekondari Mkombozi iliyoko Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro na kupangwa kidato cha tano kwenye shule ya Sckondari Namwai kuwa nafasi yake amepewa mwanafunzi mwingine hivyo yeye kukosa haki ya kuendelea na masomo.
TAMISEMI imefuatilia taarifa hizo kwa kina kutoka Mkombozi Sekondari alikosoma mwanafunzi huyo (O’ Ievel) mpaka shule ya Sckondari Namwai iliyoko Siha mkoani Kilimanjaro alikopangiwa mwanafunzi huyo kuendelea na masomo ya kidato cha tano.
Imebainika kuwa binti anayelalamika mitandoni anaitwa Sifaeli Tawel Elirehema na alisoma shule moja na Sifika Daniel Ruben. Hata hivyo binti huyo namba yake ya Mtihani ilikuwa ni S.850/135 alipata Div IV: 34 (Zero) na alisoma masomo ya Sanaa ilihali Sifika Daniel Ruben namba yake ya mtihani ni S.850/136 alisoma masomo ya Sayansi na amepata Division 1:10.
Binti anayelalamika mitandaoni alifikishwa shuleni hapo na Wazazi/Walezi kuripoti akiwa hana viambatanisho vyovyote (Result Slip) na alipohojiwa ilibainika kuwa amewadanganya walezi wake kuanzia jina mpaka matokeo yake na kwa sababu walezi hao walimchukua kama msaidizi wa nyumbani hawakufahamu ukweli wa taarifa walizopewa na binti huyo.
Kufuatia taarifa hii tunapenda kuujulisha umma kuwa hakuna mwanafunzi aliyenyang’anywa haki yake ya kuendelea na masomo ya kidato cha tano na taarifa zilizotokwa na binti huyo ni za uongo na zipuuzwe na mwanafunzi Sifika Daniel Ruben anaendelea na masomo yake Namwai Sekondari.
Aidha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Mohamed 0. Mchengerwa amewataka Wazazi/Walezi na wanaharakati kutokusambaza taarifa ambazo hawajajiridhisha na usahihi wake iii kuepuka kuzua taharuki kwenye jamii.
#KoncetTVUpdates