ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Saturday, September 23, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

TANESCO YAHIMIZWA KUBORESHA UPATIKANAJI UMEME MTWARA NA LINDI

SUZO SHUKRANI by SUZO SHUKRANI
Sep 15, 2023
in HABARI
0
TANESCO YAHIMIZWA KUBORESHA UPATIKANAJI UMEME MTWARA NA LINDI
0
SHARES
15
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

 

RelatedPosts

Maurel and Prom: Empowering Tanzania’s Sustainable Energy Economy

Maurel and Prom: Empowering Tanzania’s Sustainable Energy Economy

Sep 22, 2023

DR KONGO YATAKA MONUSCO KUONDOKA HARAKA

Sep 21, 2023

HAIER TANZANIA NA AZAM TV WAUNGANA KUKIWASHA KWA PAMOJA

Sep 21, 2023
Load More

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amelihimiza Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania – TANESCO kufanya jitihada mbalimbali kuhakikisha mikoa ya Mtwara na Lindi inapata umeme wa kutosha.

Naibu Waziri Kapinga ameyasema hayo tarehe 14/09/2023 wakati alipotembelea Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa kutumia Gesi Asilia cha Mtwara.

Kituo hicho kina mitambo 13 yenye uwezo wa kuzalisha umeme MW 30.4 lakini kwa sasa kinazalisha MW 19 kutokana na mitambo mitatu kuwa katika Matengenezo na kinahudumia mikoa ya Mtwara na Lindi.

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga ametembelea kituo hicho ili kuangalia hali halisi ya mitambo na uzalishaji wa umeme kituoni hapo ikiwa ni sehemu ya ufuatiliaji wa hali ya upatikanaji wa huduma ya umeme kwa wananchi wa mikoa ya Mtwara na Lindi.

Naibu Waziri Kapinga amemuelekeza Meneja wa Kituo hicho cha Kuzalisha Umeme kwa kutumia Gesi Asilia cha Mtwara, kuhakikisha wanafanya jitihada za kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme mkoani humo ili kukidhi hamu ya wakazi wa mikoa ya Mtwara na Lindi ya kupatiwa umeme wa kutosha.

Naibu Waziri Kapinga amesema, jukumu kubwa walilonalo nikuhakikisha kuwa Watanzania wanapata Nishati ya Uhakika.

Amesema, katika uongozi wake, kwa kushirikiana na Watumishi wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake atahakikisha, anamsadia ipasavyo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Doto Biteko kuhakikisha wanatimiza kiu ya Watanzania kupata Nishati ya Uhakika.

Naibu Waziri Kapinga ameongeza kuwa, ili azma hiyo itimie, wanahitaji kupatiwa ushirikiano kutoka kwa watumishi wa Wizara na Taasisi zake ili kwa pamoja kutekeleza mipango iliyowekwa ya kuwapatia Watanzania Nishati ya Uhakika ikiwezekana kuzidi lengo lililowekwa na Serikali kufikia 2025.

Naibu Waziri Kapinga amesema, mafanikio yake kiuongozi kwa kiasi kikubwa yatategemea ushirikiano mzuri wa Watumishi wa Wizara na Taasisi zake katika kufanya kazi kwa bidii, maarifa, moyo wa kujituma na kwa ushirikiano.

 

#KonceptTVUpdates

Related

SUZO SHUKRANI

SUZO SHUKRANI

Related Posts

Maurel and Prom: Empowering Tanzania’s Sustainable Energy Economy
BIASHARA

Maurel and Prom: Empowering Tanzania’s Sustainable Energy Economy

by I am Krantz
Sep 22, 2023
DR KONGO YATAKA MONUSCO KUONDOKA HARAKA
HABARI

DR KONGO YATAKA MONUSCO KUONDOKA HARAKA

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023
HAIER TANZANIA NA AZAM TV WAUNGANA KUKIWASHA KWA PAMOJA
HABARI

HAIER TANZANIA NA AZAM TV WAUNGANA KUKIWASHA KWA PAMOJA

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023
MNH YAFANYA UPASUAJI WA KWANZA TUNDU DOGO MOJA
AFYA

MNH YAFANYA UPASUAJI WA KWANZA TUNDU DOGO MOJA

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023
SBL KUUNGANISHA TAMADUNI KUPITIA OKTOBA FEST
HABARI

SBL KUUNGANISHA TAMADUNI KUPITIA OKTOBA FEST

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023
TAWA YATAKIWA KUJIPANGA KUONGEZA UKUSANYAJI MAPATO
HABARI

TAWA YATAKIWA KUJIPANGA KUONGEZA UKUSANYAJI MAPATO

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

September 2023
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930  
« Aug    
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In