TIRDO na REPOA imeandaa programu ya mafunzo ya utengenezaji wa Mkaa Mbadala (Biomass Briquettes) ambayo ni nishati safi kwa matumizi ya majumbani, taasisi na hata viwandani.
Mafunzo hayo yanalenga kuimarisha umuhimu Kwa ustawi wa uchumi na mazingira na afya Kwa ujumla na uzalishaji Bora wa mkaa mbadala ambao unaotumia malighafi za taka za kilimo na misitu (agricultural and forest wastes)
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jumanne Septemba 12,2023 Mkurugenzi Mkuu Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania TIRDO Prof. Mkumbukwa Mtambo amesema mikakati, na njia bora ya uzalishaji wa mkaa mbadala pamoja na upimaji ubora wa bidhaa inayozalishwa na aina ya nyenzo au mashine zinazotumika katika uzalishaji huo.
“tutaweza kujua ni kwa nini watumiaji wengi wa bidhaa unayozalisha wanabadili mawazo na kutumia nishati nyingine na sio mkaa mbadala. Ikiwa wewe ni mgeni kwenye uzalishaji huu au unatafuta kuongeza ujuzi ulionao, kozi hii inalenga kukuongezea ujuzi na ufahamu muhimu wa uzalishaji bora wa mkaa safi”Amesema Mtambo
Aidha Prof Mtambo amesema Mafunzo haya yametayarishwa baada ya kufanya utafiti katika mikoa 12 hapa nchini na kuweza kutembelea wazalishaji mkaa mbadala 58 na watumiaji 122. Utafiti huu ulifanywa na TIRDO kwa kushirikiana na REPOA ukiwa na lengo la ‘Kuimarisha Uzalishaji wa Mkaa Mbadala (Biomass Briquettes) na Kukuza Matumizi yake kwa Ajili ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi nchini Tanzania.
“Watafiti waliweza kuchukua sampuli 43 za mkaa mbadala kutoka kwa wazalishaji katika mikoa hiyo na kupima kwenye maabara ili kuangalia ubora wake. Matokeo ya upimaji huo ulipelekea TIRDO na REPOA kufanya uboreshaji mkaa huo baada ya kuwa na changamoto za viwango na ubora unaotakiwa kulingana na viwango vya nchi”. Aliongezea Prof Mtambo.
#KonceptTVUpdates