Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limepitisha ombi la pamoja la nchi za Kenya, Uganda na Tanzania kuandaa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mwaka 2027.
Ombi hilo limekubaliwa kwenye mkutano wa CAF ExCo ambao umefanyika hoteli ya Marriott, Cairo nchini Misri na kwa upande wa Tanzania imewakilishwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Damas Ndumbaro Pamoja na rais wa shirikisho la soka TFF Wallace Karia.
Kwa hatua hii sasa Tanzania itaungana na kenya Pamoja na Uganda kuandaa michuano hiyo ya AFCON ambayo mataifa ya Afrika yatachuana kuwania taji hilo, na ikumbukwe kuwa hii ni mara ya kwana kwa nchi za ukanda wa Afrika mashariki kuandaa mashindano haya.
#KonceptTVUpdates