Makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Philip isdor Mpango amesema Tanzania imeanzisha ufadhili wa gharama nafuu na ufadhili wa muda mrefu wa kilimo kwa sekta binafsi ikiwa ni pamoja na kuanzisha kituo katika Benki Kuu ambacho kinaziwezesha benki za biashara kukopa kwa ajili ya kuendelea kuwakopesha wakulima kwa riba ya tarakimu moja.
Ameyasema hayo leo septemba 5,2023 kwenye uzinduzi wa Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF 2023), katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam ambapo mkutano huo utafanyika kwa siku nne na kutamatika siku ya ijumaa tarehe 8, septemba 2023.
Katika mkutano huo Tanzania ni mwenyeji kwa mwaka huu ambapo wizara ya kilimo inaratibu mkutano huo, aidha Makamu wa rais dkt mpango ameongeza kuwa ni Lazima kufadhili mgao wetu wa idadi ya watu, rasilimali kubwa na wanawake wenye nguvu ili kufikia mabadiliko ya mifumo ya chakula.”
#KonceptTVUpdates