Waziri wa mambo ya ndani nchini Ecuador Juan Zapata amesema Wafungwa katika gereza moja mjini Cuenca nchini Ecuador wanawashikilia mateka walinzi 50 wa gereza na maafisa saba wa polisi.
Tukio hilo limetokea siku moja baada ya mamia ya wanajeshi na maafisa wa polisi kufanya operesheni ya kutafuta silaha, risasi na vilipuzi katika moja ya magereza makuu nchini humo mjini Latacunga Kusini mwa nchi hiyo.
Mapema, ofisi ya serikali inayosimamia magereza SNAI, ilisema kuwa hatua ya kuwashika mateka maafisa hao ni kisasi cha operesheni hiyo, lakini mamlaka baadaye ilisema hatua hiyo ilikuwa ni ya kupinga uhamisho wa wafungwa hadi magereza mengine.
Magereza ya Ecuador yamekuwa maeneo ya mauaji ya magenge hasimu yenye uhusiano na magenge ya Colombia na Mexico ambayo yamesababisha vifo vya wafungwa zaidi ya 430 tangu 2021.
#KonceptTVUpdates