Hii leo jumanne septemba 12,2023 baraza la mitihani Tanzania limetoa idadi ya watahiniwa wanaotarajiwa kufanya mitihani ya kuhitimu darasa la saba kwa mwaka wa 20203 ambapo watahiniwa 1,397,370 wataanza kufanya mitihani hiyo nchi nzima kesho Septemba 13 na 14.
Kati ya watahiniwa hao, 654,652 ni wavulana sawa na asilimia 46.85 na wasichana ni 742,718 sawa na asilimia 53.15.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dkt. Said Mohamed amewataka wahusika kuzingatia sheria na kujiepusha na vitendo vya udanganyifu.
Dkt. Mohamed amesema kwa wanafunzi watakaobainika kufanya udanganyifu matokeo yako yatafutwa kwa mujibu wa kanuni za mitihani na wahusika wengine watachukuliwa hatua za kwa mujibu wa sheria.
“Tunaamini wanafunzi wameandaliwa vyema katika kipindi chote cha miaka saba, hatutegemei kuona watahiniwa wanafanya udanganyifu kwa kuwa tutawafutia matokeo. Si kitu tunachokipenda kuona mtoto amesoma miaka saba halafu anafutiwa matokeo,” amesema Dkt Mohamed.
#KonceptTVUpdates