Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amebainisha kuwa zaidi ya watoto laki Nne wanatarajia kupata chanjo dhidi ya ugonjwa wa Polio katika Mkoa wa Songwe.
Waziri Ummy ameyasema hayo Septemba 11, 2023 wakati akianza ziara yake ya kukagua huduma zinazotolewa katika Halmashauri ya Wilaya ya Songwe ambapo ameanza kutembelea katika Hospitali ya Wilaya hiyo, Zahanati ya Mbala pamoja na Kituo cha Afya Mbuyuni kilichopo katika Wilaya hiyo.
“Baada ya kupatikana kwa mtoto Mmoja mwenye ugonjwa wa Polio tumeamua kutoa chanjo ya ugonjwa huo ambapo kwa Mkoa wa Songwe tunatarajia kuchanja watoto takribani Laki Nne ambao wana umri chini ya Miaka Nane”. Amesema Waziri Ummy
Amesema, Mwaka 2015 Shirika la Afya Duniani (WHO) iliitangaza Tanzania kuwa ni nchi ambayo imetokomeza ugonjwa Polio, Mwaka huu 2023 Tanzania imepata Mtoto mwenye ugonjwa huo katika Manispaa ya Sumbawanga Mkaoni Rukwa.
#KonceptTVUpdates