Waziri wa Nchi. Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Milaa Mhe. Mohamed 0. Mchengerwa amemuelekeza Katibu Mkuu OR-TAMISEMI kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi 7 wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale mkoani Lindi kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo hivyo kuzorotesha utendaji kazi wa shughuhuli mbalimball za Halmashauri hiyo.
Mhe. Mchengewa amechukua uamuzi huo wakati wa ziara katika Wilaya ya Liwale ya kukagua na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Waziri Mchengerwa ameelekeza hatua za kinidhamu zichukuliwe kwa mujibu wa Kanuni ya 42 ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2022 inayoalnisha kuwashusha vyeo. kukatwa mshahara kwa asilimia 15 kwa muda usiopungua miaka 3 pamoja na kufukuzwa kazi iwapo watabainika kufanya makosa hayo.
Watumishi wanaotalowa kuchukuliwa hatua hizo za kinidhamu ni:
- Sisty Njau – Kaimu Mhandisi wa Wilaya
- Damasi Mumwi – Mkuu wa Idara ya Maliasili
- Mustafa Magembe – Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika
- Vinsent Moyo – Mkuu wa Idara ya Ugavi na Ununuzi
- Mohamedi Songoto – Mkuu wa Idara ya TEHAMA
- Sadick Bakari Khatibu – Katibu wa Afya
- Tunu Mtamaha Afisa Ugavi na Ununuzi aliyehamishiwa Halmashauri ya Wilaya Kilwa.
Aidha. Mhe. Waziri ameelekeza kuanzia sasa Maafisa wote wenyo kesi za rushwa na ubadhirifu wasihamishwe vituo vyao vya kazi mpaka mashauri yao yanapokamilika.
“Afisa yeyote mwenye kesi ya uhujumu uchumi au ubadhirifu wakati kesi yake ikiendelea ataendelea kuchunguza mienendo yake na hukumu yake ilutoka hatopewa tena jukumu la Ukuu wa Idara au Kitengo hadi mienendo yake itakaporidhisha” amesema Waziri Mchengerwa.