Watuhumiwa watatu Salimu Ramadhani Magembe, Daudi Hosea Malugu na Abubakari Shabani Maloda wametiwa hatiani kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 Jela.
Kosa hilo lilitendwa na watuhumiwa hao Disemba 21, 2022 huko katika Kijiji cha Balangai Kata ya Funta Tarafa ya Bumbuli katika wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga kwa uvamizi wa nyumba na kisha kumtishia kwa kisu Mussa Binuri Amiri miaka 18, Mkazi wa Kijiji cha Balangai Kata ya Funta na kuiba fedha taslimu Tsh 4.1M ambazo zilikuwa katika chumba cha baba yake.
Hukumu hiyo imetolewa mbele ya Mhe. Hakimu Masewa Kavumo Septemba 12, 2023 katika Mahakama ya Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga.
Watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani hapo Januari 11, 2022 na shauri lao kupewa namba 23, 2022.
Aidha mahakama hiyo imemuachia huru mtuhumiwa wa nne ambae alikuwa ameunganishwa katika kesi hiyo ambaye ni Ally Hatibu Mchangasho baada ya kutopatikana na hatia.
#KonceotTVUpdates