ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Saturday, September 23, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

WAZIRI MAJALIWA ATAKA ONGEZEKO USHIRIKI WA WAHANDISI WAZAWA KWENYE UJENZI WA MIRADI

SUZO SHUKRANI by SUZO SHUKRANI
Sep 15, 2023
in HABARI
0
WAZIRI MAJALIWA ATAKA ONGEZEKO USHIRIKI WA WAHANDISI WAZAWA KWENYE UJENZI WA MIRADI
0
SHARES
11
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

 

RelatedPosts

Maurel and Prom: Empowering Tanzania’s Sustainable Energy Economy

Maurel and Prom: Empowering Tanzania’s Sustainable Energy Economy

Sep 22, 2023

DR KONGO YATAKA MONUSCO KUONDOKA HARAKA

Sep 21, 2023

HAIER TANZANIA NA AZAM TV WAUNGANA KUKIWASHA KWA PAMOJA

Sep 21, 2023
Load More

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Wakala ya Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kuchukua hatua za makusudi kuhakikisha wahandisi wazawa wanashiriki kwenye ujenzi wa miradi mbalimbali nchini.

Amesema kuwa kupitia utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa Tanzania, unaolenga kupunguza ukosefu wa ajira kutoka 9% hadi 8% ifikapo 2025/26, Serikali inatarajia kutimiza azma yake ya kuhakikisha inazingatia ushiriki wa Watanzania kwenye sekta ya ujenzi ili kukuza ujuzi.

Ameyasema hayo Alhamisi Septemba 14, 2023 alipomuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye maadhimisho ya siku wahandisi, katika ukumbi wa Mlimani city, Dar es Salaam.

“Wizara ya Ujenzi pamoja na bodi ya wahandisi inalifanyia kazi suala la ushiriki mdogo wa wazawa katika miradi ya maendeleo, hii ni changamoto ambayo mmeiibua, Serikali sasa imeliweka kwenye mpango wa kuhakikisha changamoto inafanyiwa kazi ili kuongeza idadi ya wazawa kushiriki katika kazi za ndani”

 

Amesema kuwa Serikali imedhamiria kuhakikisha wahandisi wazawa wananufaika kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali “miradi hii ni fursa kwenu, natoa rai mjipange na kufanya juhudi za makusudi kila mmoja kwenye eneo lake ahakikishe kwa uzalendo alionao na mapenzi kwa nchi yake kuwa kinara katika sekta unayosimamia ili kulijenga taifa letu”

Aidha, Waziri Majaliwa ameielekeza Bodi ya Usajili wa Wahandisi iandae mpango mahsusi wa kuwaendeleza wahandisi wanawake ili waweze kusajiliwa kwa wingi zaidi wanapohitimu masomo “Suala hili litekelezwe kwa ushirikiano na wadau wengine wa uhandisi”

Naye Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenye amesema kuwa Serikali inatambua mchango wa taaluma ya uhandisi katika sekta mbalimbali za kiuchumi kupitia uanzishaji wa viwanda, uendelezaji wa miundombinu ya kilimo, nishati, maji, uvuvi, utumiaji mzuri wa rasilimali na malighafi, usafiri na mawasiliano

#KonceptTVUpdates

Related

SUZO SHUKRANI

SUZO SHUKRANI

Related Posts

Maurel and Prom: Empowering Tanzania’s Sustainable Energy Economy
BIASHARA

Maurel and Prom: Empowering Tanzania’s Sustainable Energy Economy

by I am Krantz
Sep 22, 2023
DR KONGO YATAKA MONUSCO KUONDOKA HARAKA
HABARI

DR KONGO YATAKA MONUSCO KUONDOKA HARAKA

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023
HAIER TANZANIA NA AZAM TV WAUNGANA KUKIWASHA KWA PAMOJA
HABARI

HAIER TANZANIA NA AZAM TV WAUNGANA KUKIWASHA KWA PAMOJA

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023
MNH YAFANYA UPASUAJI WA KWANZA TUNDU DOGO MOJA
AFYA

MNH YAFANYA UPASUAJI WA KWANZA TUNDU DOGO MOJA

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023
SBL KUUNGANISHA TAMADUNI KUPITIA OKTOBA FEST
HABARI

SBL KUUNGANISHA TAMADUNI KUPITIA OKTOBA FEST

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023
TAWA YATAKIWA KUJIPANGA KUONGEZA UKUSANYAJI MAPATO
HABARI

TAWA YATAKIWA KUJIPANGA KUONGEZA UKUSANYAJI MAPATO

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

September 2023
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930  
« Aug    
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In