Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Ukonga Dar es salaam ametangaza kusimamisha ujenzi holela wa Vituo vya mafuta na kuzuia vibali vyote vya ujenzi wa vituo hivyo kuanzia tarehe ya uapisho wake septemba 1,2023 Nchini Tanzania na kutaka ujenzi wowote unaofanywa kuanzia sasa kuzingatia sheria ya kutovisonganisha vituo.
Waziri Silaa ameyasema hayo jana septemba 4,2023 kwenye ofisi za makao makuu ya wizara hiyo jijini Dodoma wakati wa mkutano wake na Watendaji wa Wizara hiyo ikiwa ni siku yake ya kwanza Ofisini toka aapishwe kuwa Waziri.
Waziri Silaa ameongeza na kusisitiza kuwa Vituo vya ndani ya Mji vijengwe kwa kuafuata sheria za umbali wa kituo kimoja Kwenda kingine kwa kufuata umbali wa mita mia mbili kati ya kituo kimoja hadi kingine.
#KonceptTVUpdates