Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa hii leo oktoba 2,2023 amesema uwanja wa ndege Zanzibar unahudumia ndege nyingi kuliko uwanja wa Dar es Salaam kwani ni uwanja ambao upo bize Zaidi na mizigo mingi Zaidi ya Dar es salaam, huku akisisitiza kuwa anga bado halijajaa kupokea ndege zaidi.
Ameyasema hayo hii leo alipofanya mkutano nawaandishi wa Habari juu ya ujio wa ndege mpya siku ya kesho huku akisema kuwa kwenye viwanja vikubwa vya ndege duniani kila baada ya dakika tano hupokea ndege ikiwa ni tofauti na upande wetu hapa nchini ambapo kuna uwezekano wa kukaa Zaidi ya saa moja bila ya kupokea ndege aina yoyote.
Aidha Waziri Pro. Mbarawa amesema kuwa “Kuja kwa ndege hii kutapunguza hasa ucheleweshaji. Air Tanzania tumewaelekeza sana waende wakawasiliane na wateja wao. Tanzania watu wengi wanaipenda Air Tanzania… ndege inaweza kuchelewa lakini jinsi gani unavyomfahamisha mteja wako ndio muhimu.”
#KonceptTVUpdates