Takriban wahamiaji 10 wameuawa na wengine 25 kujeruhiwa baada ya lori la mizigo lililokuwa limewabeba kwa siri kupinduka kwenye barabara kuu kusini mwa Mexico.
Ajali hiyo ilitokea mapema Jumapili katika jimbo la Mexico la Chiapas karibu na mpaka na Guatemala.
Chanzo katika ofisi ya mwendesha mashtaka ambacho kilizungumza kwa msingi wa kutotajwa jina kiliambia shirika la habari la AFP kuwa waasiriwa hao wanatoka Cuba na wote walikuwa wanawake, akiwemo mtoto mmoja.
Tukio hilo lilitokea kwenye barabara kuu kando ya pwani ya Pasifiki kati ya miji ya Pijijiapan na Tonala, ambapo mara nyingi watu husafiri wanapojaribu kufika Marekani.
Maelfu ya wahamiaji kutoka nchi mbalimbali husafiri kote Mexico kwa mabasi, trela na treni za mizigo wanapoelekea Marekani.
#KonceptTVUpdates