Kutoka kushoto Afisa Maendeleo ya Biashara wa Vodacom Tanzania, Kelvin Donald akiwa na Afisa Masoko, Nancy Emmanuel pamoja na Mkaguzi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Pendo Mfuru na Afisa Masoko, Fredrick Mwamyalla upande wa kulia wakiwa katika droo ya kwanza kampeni ya msimu wa sikukuu ijulikanayo kama ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’ iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kupitia droo hiyo jumla ya washindi 26 walipataka kwa kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo bodaboda, luninga, simu za mkononi, router za 4G na 5G ambapo mteja mmoja mwenye bahati alijishindia pesa taslimu kiasi cha shilingi milioni 10!